AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KIGOMA

AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KIGOMA
Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma katika kesi ya Jinai Na. 01/2021 mbele ya Jaji A. Matuma imemuhukumu mshtakiwa Alfred Kwezi kunyongwa hadi kufa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la mauaji ya kukusudia.
Mshtakiwa Alfred Kwezi alishitakiwa kwa kosa la mauaji ya kukusudia baada ya kumuua Godfrey Ndayate kwa kumshambulia na mapanga na kukata kichwa na kukitenganisha na mwili
Hukumu hiyo ilitolewa baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri dhidi ya mshitakiwa pasipo kuacha shaka na kuthibitisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo ambapo mtuhumiwa alihukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa hilo la mauaji ya kukusudia.
Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kwa kumkatakata kwa mapanga na kisha kutenganisha kichwa chake na kiwiliwili, ambapo kitendo hicho ni kinyume cha sheria za nchi.
Kesi hiyo iliendeshwa na Mawakili wa Serikali Benedict Kivuma na Raymond Kimbe