Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

51 WAFUTIWA MASHTAKA MANYARA DPP AWATAKA WASIRUDIE MAKOSA
27 Nov, 2020
51 WAFUTIWA MASHTAKA MANYARA   DPP   AWATAKA WASIRUDIE MAKOSA

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga jana tarehe 26 Novemba amesikiliza na kuwafutia Kesi watu 51 wakiwepo wanaume arobaini na tisa na wanawake wawili waliokuwa katika gereza la Babati mkoani Manyara.

Bw.Mganga Baada ya kuwafutia Mashtaka aliwataka wakirudi uraiani kuwa raia wema na kutorudia kutenda makosa.