Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Watuhumiwa 95 wamefutiwa mashtaka katika gereza la Geita
07 Sep, 2020
Watuhumiwa 95 wamefutiwa mashtaka katika gereza la Geita

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Biswalo Mganga mnamo tarehe 6 Septemba, 2020, amewafutia mashtaka watuhumiwa 95 katika gereza la Wilaya ya Geita.

Bw. Biswalo Mganga amewafutia mashtaka watuhumiwa hao baada ya kutembelea gereza hilo na kujionea hali halisiya uendeshajiwa gereza hilo ambapo pia alipata nafasi ya kulikagua na kuwasikiliza mahabusu na wafungwa waliokuwepo katika gereza hilo.

Miongoni mwa watuhumiwa aliowaachia huru ni wale wenye makosa madogo, ambao ushahidi wake ni dhaifu, wazee na vijana wenye umri chini ya miaka 18 ambao aliwafutia mashtaka baada ya kuwahoji.

Katika ziara hiyo Bw. Biswalo Mganga aliongozana na wajumbe wa Kamatiya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Geita.

Akizungumza na watuhumiwa hao, Mkurugenzi wa Mashtaka aliwataka kuacha kutenda maovu na kuwa raia wema.