Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

​WASHTAKIWA 467 WAANDIKA BARUA ZA KUOMBA KURUDISHA SHILINGI BILIONI 107 NA MILIONI 842 – DPP MGANGA
01 Oct, 2019
​WASHTAKIWA 467 WAANDIKA BARUA ZA KUOMBA KURUDISHA SHILINGI BILIONI 107 NA MILIONI 842 – DPP MGANGA

WASHTAKIWA 467 WAANDIKA BARUA ZA KUOMBA KURUDISHA SHILINGI BILIONI 107 NA MILIONI 842 – DPP MGANGA

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Biswalo Mganga amewasilisha taarifa ya msamaha kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi nchini kwa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli na kusema kuwa washtakiwa 467 wameandika barua za kuomba kurudisha jumla shilingi Bilioni 107 na Milioni 842.

DPP Mganga amefafanua kuwa kati ya fedha hizo wapo washtakiwa waliotayari kulipa hivi sasa kiasi cha shilingi Bilioni 13 na Milioni 602 pamoja kukabidhi Serikalini madini yakiwemo dhahabu na Tanzanite yenye jumla ya kilo 35, na pia wapo washtakiwa waliotayari kulipa shilingi Bilioni 94 na Milioni 240 kwa awamu.

Ameongeza kuwa pamoja na fedha hizo, wapo washtakiwa wengine wawili walioitikia zoezi hilo na hivyo kukiri makosa yao Mahakamani ambapo mmoja wao amelipa shilingi Bilioni 1 na Milioni 37 na amekabidhi Serikalini gramu 2,123.64 za madini ya vito yenye thamani ya shilingi Milioni 36.5.

DPP Mganga amemuomba Mhe. Rais Magufuli aongeze siku kwa watuhumiwa kuwasilisha barua zao za kuomba msamaha na kurejesha fedha na mali kutokana na baadhi yao kushindwa kufanya hivyo kwa kipindi kifupi cha siku 7 kutokana na sababu mbalimbali.