Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Washitakiwa 25 waachiwa huru katika gereza la Nzega
20 Aug, 2020
Washitakiwa 25 waachiwa huru katika gereza la Nzega

Washitakiwa Ishirini na tano waliokuwa wamewekwa katika gereza laNzega lililopo wilaya ya Nzega Mkoa Tabora mnamo 18/8/2020 wameachiwa huru na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga baada ya kutembelea gereza hilokujionea hali halisi ya uendeshajina kusikiliza malalamiko ya washitakiwa.

Akizungumza na washitakiwa hao Bw. Mganga aliwataka washitakiwa kuacha kutenda uovu na kufanya yaliyo mema ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya uhalifu.

“ Mtu yeyote asiwashawishi kujihusisha na vitendo vya uhalifu wala kufanya fujo ya aina yeyote na wakati wote msikubali kudanganywa” alisisitiza Bw. Mganga.

Miongoni mwa majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka ni kukagua magereza na mahali popote wanapohifadhiwa wahalifu kwa mujibu wa sheria.