Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

UPELELEZI MZURI NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTOAJI HUKUMU YA HAKI - DPP
01 Mar, 2022
UPELELEZI MZURI NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTOAJI HUKUMU YA HAKI - DPP

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. SylvesterMwakitalu amesema Upelelezi mzuri ni nguzo muhimu katika kuhakikisha kuwa hukumu inatolewa vizuri na kwamba usipofanyika vizuri wahalifu hawataweza kupatikana.

“ Upelelezi usipofanyika vizuri hakuna namna Mwendesha Mashtaka ataendesha kesi vizuri. Uchunguzi na upelelezi wa mali lazima ufanyike vizuri ili kupelekea mashtaka kuandaliwa vizuriili mhalifu asinufanikekwa mali alizozipata kwa njia ya uhalifu.Mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu zitafutwe, zifuatiliwe na zitaifishwe ili kuhakikisha kuwa uhalifu unakomeshwa na kuwapa taarifa wahalifu kuwa uhalifu haulipi. Alisisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka.

Bw. Mwakitalu alisemaMaendeleo ya Sayansi na Teknolojia yanawarahisishia Wahalifu kufanya uhalifu, kuficha na kuzitakatishakutokana na uhalifu kufanyika katika mifumo yakiektroniki hivyo inabidi kutobaki nyuma na kuhakikisha Waendesha Mashtaka na Wapelelezi wanajengewa uwezo ili waweze kudhibiti uhalifu.

Alisema ni matarajio yake kuwa mafunzo wanayoyapata yanatarajiwa kuwa na matokeo bora na kuboresha utendaji kazi. “ kufundisha watu sabini na tano tu siyo jambo kubwa ila ninachotaka kukipata baada ya mafunzo haya ni kuona maboresho yakitokea katika utendaji kazi na kuona namna uendeshaji wa mashtaka unavyobadilika na kuendeshwa kwa weledi na kuhakikisha kuwa majalada yanayofikishwa mahakamani yanakuwa na ushahidi unaojitosheleza kwa kuwa na mashtaka kamili badala ya kuwa na ushahidi wa kuungaunga.

Alisema kumekuwa na changamoto na kelele nyingi namanung’uniko juu ya taratibu za Makubaliano ya Kukiri Kosa( Plea-Bargaining) kwa kuwa ni utaratibu mpya lakini ni mzuri ambao ukitumika vema utasaidia kupunguza msongamano wa mahabusu na wafungwa hivyo alisema mafunzo yanayotolewa yatawezesha kuboreshwa kwa utaratibu huo.

“ Nategemea mkitoka hapa kwenye mafunzo kuhusu Utaratibu wa Makubaliano ya Kukiri Kosa ( Ple- bargaining) mtaenda kufanya kazi kwa weledi na pia nahitaji mjitahidi kujifunza kwa bidii ili muweze kufanya kazi vizuri katika eneo hilo.

Akifungua Mafunzo juu ya taratibu za Kisheria za Utaifishaji Mali na Makubaliano ya Kukiri Makosa kwa waendesha Mashtaka na Wapelelezi kwa Waendesha Mashtaka na wapelelezi kuanzia tarehe 28 Februari, 2022 hadi Machi 4 Machi, 2022 Bw. Mwakitalu alisema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imepewa jukumu kubwa la kuhakikisha nchi inakuwa na amani na utulivu hivyo aliwataka Waendesha Mashtaka na Wapelelezi kufikisha ujumbe kwa wahalifu kuwa uhalifu haulipi kwa kufanya kazi kikamilifu.

Alilishukuru Shirika lisilo la Kiserikali la PAMS foundation kwa kuona umuhimu wa kufadhili mafunzo na tafiti mbalimbali kwa watumishi wanaopambana na uhalifu.

Aidha, aliwataka kuzingatia mafunzo wanayoyapata na kuyapa uzito unaostahilikwakuwa Waendesha Mashtaka na Wapelelezi ni watu muhimu katika suala zima la utoaji wa Haki Jinai.

Mkurugenzi wa Mashtaka pia alitumia nafasi hiyo Kumshukuru JajiMkuu wa Tanzania Mhe. Ibrahim Juma na Mahakama ya Tanzania kwa kukubali kutoa Waheshimiwa Majaji , Mahakimu na Wasajili kushiriki katika mafunzo kwa kutoa mafunzo(mada) kwa kwani kuwa nao ni nafasi adhimu na isiyoweza kupatikana kwa urahisi utokana na majukumu waliyonayo na piauzoefu walionao wanapoutoa utasaidia kurekebisha makosa yanapojitokeza.

Mafunzo Mafunzo juu ya taratibu za Kisheria za Utaifishaji Mali na Makubaliano ya Kukiri Makosa kwa Waendesha Mashtaka na Wapelelezi kuanzia tarehe 28 Februari, 2022 hadi Machi 4 Machi, 2022 yameandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kufadhiliwa na Shirika Lisilo la Kiserikali la PAMS.