Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Shilingi Milioni 35 zalipwa kwenye akaunti ya Serikali baada ya watuhumiwa kutiwa hatiani
26 Aug, 2020
Shilingi Milioni 35 zalipwa kwenye akaunti ya Serikali baada ya watuhumiwa kutiwa hatiani

Mahakama ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu tarehe 24 Agosti,2020 katika shauri laUhujumu Uchumi1/2018kati ya Jamhuri dhidi ya LemaJeremiahna wenzakewatatuambao awali walikuwa wameshtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya madarakana kusababisha hasara ya kiasi cha shilingi 30,721,300/= kwa Mamlaka ya Maji Maswa imewatia hatiani washtakiwa hao kwa kosa la udanganyifu na kuwaamuru kulipa kiasi cha shilingi 35,721,300/= kama fidia kwa Serikalina faini ya kiasi cha shilingi 380,000/= kila mmoja au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Washtakiwa hao wamelipa kiasi cha shilingi 35,721,300/= kwenye akaunti ya Serikaliya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP)kama walivyoamuriwa na mahakama.