Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

Ni kikao cha kihistoria- DPP
02 Jul, 2021
Ni kikao cha kihistoria- DPP

Na Rebecca Kwandu, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka- Dodoma.


Ni Kikao cha Kihistoria- DPP

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amesema kikao cha pamoja kilichofanywa kati ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar jijini Dodoma tarehe 02 Julai,2021 ni kikao cha Kihistoria- kwakuwa kitatengeneza dira ya utekelezaji majukumu ya Ofisi hizo hususani katika masuala ya Upelelezi,,uratibu wa Upelelezi na Uendeshaji wa Mashtaka okie kuboresha utoaji Haki Jinai nchini.

Akifungua kikao cha Menejimenti za Ofisi ya Mashtaka, Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa jijini Dodoma leo amesema kikao hicho kitawezesha kupatikana kwa mikakati mizuri ya utendaji wa kazi.

" Katika kikao hiki tutaweka mikakati vizuri, tutapokea michango kutoka kwa wajumbe na maazimio yatapatikana alisema Mkurugenzi Mwakitalu.

Alisema zipo kesi nyingi ambazo zimechelewa kuisha kutokana na sababu mbalimbali hivyo ni matumaini yake kuwa kikao hiki kitajadili kwa kina na kutoka na suluhisho la kutatua changamoto zinazopelekea kesi kuchelewa.

" Maazimio ya kikao chetu yatapelekwa kwa viongozi wetu wa Mikoa ili wayajadili na kuyafanyia kazi ili kuleta matokeo kwenye utendaji wao.
" Tutatengeneza dira nzuri,tutawapa mwongozo viongozi wetu wa Mikoa ili mashauri yaende kwa haraka" alisema Mkurugenzi Mwakitalu.
Kikao cha Jukwaa la Haki Jinai cha Menejimenti za Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kimefanyika jijini Dodoma tarehe 02 Julai,2021.