Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

MKURUGENZI WA MASHTAKA NCHINI AWAHAKIKISHIA UPATIKANAJI WA HAKI WAKAZI WA MUFINDI
23 Oct, 2020
MKURUGENZI WA MASHTAKA NCHINI AWAHAKIKISHIA UPATIKANAJI WA HAKI WAKAZI WA MUFINDI

Mkurugenzi wa Mashtaka nchiniBw Biswalo Mganga amesema kuwa haki kwa wakzi wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa itapatikana kwawakatikutokana na kusogezewa huduma karibu yao baada ya uzinduzi wa ofisi ya taifa ya mashtaka katika makao makuu ya Wilaya hiyo yaliyopo Mjini mafinga

Biswalo ameeleza hayo wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilayani humo, ikiwa ni lengo la ofisi hiyo kusogeza huduma karibu na wananchi .

Aidha Bw. Mganga ameongeza kuwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi ni kuwa na utawala bora, kulinda haki na amani kwa kila Mtanzania na kupunguza malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wananchi walio wengi na kuahidi kuwashughulikia wale wote ambao wanavuruga usalama wa nchi.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri amepongeza jitihada hizo kwa kuhakikisha Ofisi hiyo inafunguliwa Wilayani humo ambapo amesema kufunguliwa kwake imekuwa faraja kubwa kwa wananchi wa Mafinga

Jamhuri ameongeza kuwa wananchi wake watapata elimu ya kutosha juu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, kuhusiana na kazi inazozifanya na kuhakikisha haki inatendeka baina ya wananchi huku akiwaasa wananchi wa wilaya hiyo kuitumia vema i Ofisi hiyo sanjari na kutoa ushirikiano ipasavyo.

Kwa upande wake mmoja wa wananchi waliohudhuria hafla hiyo ameishukuru na kuipongeza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu zaidi na kuwa itasadia kupunguza mudauliokuwa ukitumika kupata haki zao

Naye pia Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Edson Makallo ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya waendelea kujitolea maeneokwa ajili ya shughuli za ofisi hiyo iweze kuendeshaji wa Mashtaka kwani Ofisi zilizopo ni chache.

Aidha ameongeza kuwa hadi saa tumefanikiwa kufungua jumla ya Ofisi za Wilaya 15, ukizingatia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka zinapaswa kuenea jumla ya Wilaya 139".