Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Mkazi wa Babati ahukumiwa miaka 20 jela kwa kukutwa na nyama ya pundamilia
27 Aug, 2020
Mkazi wa Babati ahukumiwa miaka 20 jela kwa kukutwa na nyama ya pundamilia

Mahakama ya Wilayaya Babati Mkoani Manyarakatika kesi ya Uhujumu Uchumi Na. 20/2020 imemuhukumu kwenda jela miaka ishirini mshtakiwa Salim Kijuu kwa kosa la kukutwa na Nyara za Serikali ambazo ni Nyama ya Pundamilia yenye uzito wa kilo 17.5, kinyume cha kifungu cha 86(1), 2(b) cha Sheria ya Uhifadhi wa WanyamaporiNa.5 ya mwaka 2009 kikisomwa pamoja na Aya ya 14 ya jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 3septemba 2019 katika kijiji cha Gidejabong kilichopo Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara

Mshtakiwa Salim Kijuu ana umri wa miaka 38 na mkazi wa kijiji cha Gidejabong kilichopo Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara.

Katika kesi hiyo upande waMashtaka uliwasilisha mahakamani mashahidi watano na vielelezo 7 na upande wa utetezi ulikuwa na shahidi mmoja.

Mshitakiwa amepatikana na hatia na Mahakama imemwamuru kutumikia kifungo cha miaka 20 na kielelezo alichokutwa nacho kutaifishwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa Mkurugenzi wa maliasili

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa tarehe 03 septemba 2019 na hukumu imetolewa leo tarehe 26 Agosti 2020 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Babati Mhe. Victor Kimario ambapo upande wa Mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Timotheo Mmari na mwendesha Mashtaka wa TANAPA Rasticus Mahundi.