MIKOA 15 YAIBUKA VINARA WA USHINDI NA UMALIZIAJI WA KESI
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu, amekabidhi jumla ya kompyuta mpakato (laptop) 15 kwa mikoa ya kimashtaka 15 iliyofanya vizuri katika wastani wa ushindi wa kesi (conviction rate) na wastani wa umaliziaji wa kesi (disposal rate).
Akizungumza wakati wa kuhitimisha Mkutano Mkuu wa kwanza wa Mwaka wa Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, DPP Mwakitalu amesema kuwa utoaji wa laptop hizo ni njia ya kutambua na kuthamini juhudi za mikoa iliyofanya vizuri, sambamba na kuongeza hamasa ya uwajibikaji kwa mikoa mingine ili nayo iboreshe utendaji wake katika maeneo hayo muhimu.
Mikoa hiyo imefanya vizuri katika kipindi cha Januari hadi Desemba 18, 2025, ambapo Mkoa wa Mtwara umeongoza kwa kushika nafasi ya kwanza,ukifuatiwa na Simiyu , Nafasi ya tatu imeshikiliwa na Mkoa wa Kilimanjaro.
Mikoa mingine ni Mwanza iliyoshika nafasi ya nne, Rukwa nafasi ya tano , Lindi nafasi ya sita, Manyara nafasi ya saba, Katavi nafasi ya nane, Shinyanga imefika nafasi ya tisa na singida nafasi ya 10.
Aidha, mikoa mingine iliyofanya vizuri ni Tanga nafasi ya 11, Kagera nafasi ya 12, Mara nafasi ya 13, Arusha nafasi ya 14 na, huku Njombe ikishika nafasi ya 15.
Kutolewa kwa zawadi hizo ni ishara ya kuimarisha ari ya kazi, kwa kuhakikisha kwamba watumishi wote wanatekeleza majukumu yao kwa weledi, uwajibikaji na uaminifu wakati wote, kwani wao ndiyo nguzo na tegemeo kuu la maendeleo ya taifa.