Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

KAIMU NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA AISHUKURU UNICEF
15 Nov, 2021
KAIMU NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA AISHUKURU UNICEF


Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji wa Kesi Bi. Neema Mwanda amelishukuru Shirika la Kimataifa la Watoto (UNICEF) kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika kufadhili Mafunzo na maelekezo ya utekelezaji wa ukaguzi wa vizuizi vya watoto wanaokinzana na sheria wakishirikiana na timu ya maandalizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo yamefanyika leo tarehe 15 Novemba, 2021 katika Ukumbi wa Rafiki Hotel Jijini Dodoma.

"Elimu mnayopata hapa mkawape na wenzenu, msikae kimya kwani haitaleta tija katika utendaji wa kazi zetu. Na pia mkifika mkawe waalimu wa Mawakili wenzenu mliowaacha ili kesi za watoto ziweze kuendeshwa kwa ufanisi mkubwa na weledi."

Alizungumza hayo Bi. Neema Mwanda wakati akitoa neno la kufunga mafunzo hayo.

Nae pia Mratibu wa Ulinzi na Usalama wa Mtoto kutoka Shirika la Kimataifa la Watoto (UNICEF) Bi. Victoria Mgonela ametoa shukrani kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kueleza jinsi wanavyoshirikiana kikamilifu na ofisi hiyo katika kushughulikia mashauri ya watoto.