DPP AWATAKA MAKATIBU SHERIA KUFUATA MAADILI YA KAZI.
DPP AWATAKA MAKATIBU SHERIA KUFUATA MAADILI YA KAZI.
17 Dec, 2021
- Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amewataka Makatibu Sheria kufanya kazi zao kwa kuzingatia miiko na misingi ya utumishi wa umma.Mkurugenzi Mwakitalu ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu Sheria kutoka Mikoa na Wilaya mbalimbali nchini kilichoanza leo tarehe 17 hadi 18 Disemba, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.Bw. Mwakitalu aliendelea kuwaasa Makatibu Sheria kuwa baada ya kumaliza kikao kazi hiki wanapaswa kubadilika na kwenda kufanya kazi zao kwa uadilifu, na kwa moyo wa kujituma."Tumekabidhiwa dhamana Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, tucheze kama timu moja, tufanye kazi kwa kushirikiana ili kwa pamoja tusimame na tusonge mbele. Pamoja na changamoto mbalimbali tulizonazo lakini tujitahidi kufanya kazi kwa bidii." Amezungumza hayo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.Nae pia Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji wa Kesi Bi. Neema Mwanda alieleza kuwa lengo kuu la kikao kazi hiki ni kujifunza na kuongeza uelewa zaidi juu ya masuala mbalimbali ya kiutendaji katika kazi zinazofanywa na Makatibu Sheria, hivyo basi kupitia kikao kazi hiki ana mategemeo ya kuwa washiriki wote watatoka wakiwa wameongeza uelewa zaidi katika kazi zao tofauti na walivyokuja.