Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE
24 Oct, 2020
MKURUGENZI WA MASHTAKA  AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA VURUGU ASEMA NCHI  INAPASWA KUWA SALAMA WAKATI WOTE

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mgangaameeleza"Yeyote atakayefanya fujo kipindi hiki ama kipindi chochote kile waache mara moja, kwani serikali haiwezi kuwavumilia hao wote waliopanga kufanya fujo".

Aidha Katika hatua nyingine Bw. Mganga ameongeza kuwa tayari watu 24 Tunduma Mkoani Songwe wametiwa mbaroni kutokana na kujihusisha na vurugu zilizosababisha mauaji ya kijana mmoja mpakani hapo.

Ameyasema hayowakati wa ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Songwe.

Mkurugenzi wa Mashtaka aliendelea kueleza kuwa amewahakikishia upatikanaje wa haki baina ya wananchi Mkoani Songwe huku akisisitiza kuwa kutokana na Mkoa huo upo mpakani hivyo atahakikisha wanafungua Ofisi nyingine mpakani Tunduma kwa lengo la kuzuia uhalifu wa kimpaka

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangala alimpongeza Mkurugenzi wa Mashtaka pamoja Ofisi yake kwa kazi kubwa wanayoifanyakatika kuhakikisha haki, amani vinapatikana katika nchi hii.

Akiendelea kueleza kuwa licha ya Mkoa wa Songwe kuwa ni mchanga lakini uhitaji wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ulikuwa ni mkubwa kutokana na Mkoa huo kuwa upo mpakani na una mwingiliano mkubwa wa watu, hivyobasi uwepo wa Ofisi hiyo kuwa karibu utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kupunguza malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na wananchi juu ya ucheleweshaji wa upatikanaji wa haki.

Naye pia Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Songwe Bw. Kassim Mkwawa ameeleza kuwa uwepo wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Songwe utarahasisha majadala ya kesimbalimbali za uchunguzi kushughulikiwa kwa haraka, ambapo awali yalikuwa yakipelekwa Mbeya na kutumia muda mrefu kufanyiwa kazi.

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo pia ametoa shukrani kwaviongozi wa dini kwa namna wanavyoliombea Taifa pia amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Songwejuu ya Mtumishi yeyote wa Serikali atakaebainikakujihusisha na vitendo vya rushwa Ofisi yake haitosita kusaini barua ya kumsimamisha kazi, Kwan kufanya hivyo ni kukandamiza haki za watu wengine.

Baadhi ya wadau Mkoani Songwe wamesema uwepo wa Ofisi hiyo ni kupunguza umbali wa kupata huduma na kuondoa malalamiko baina ya wananchi.

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imewahakikishia wananchi wa Mkoani Songwe kutenda haki na kuwaondolea malalamiko ambayo yalikuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu kutokana na ukosefu wa ukaribu wa huduma za kiofisi katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani.