Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

DPP ASISITIZA UMAKINI NA WELEDI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA KIOFISI
18 May, 2022
DPP ASISITIZA UMAKINI NA WELEDI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA KIOFISI

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amewataka Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kufanya kazi kwa umakini na kwa weledi ili kuweza kulinda haki na amani za Watanzania hususani katika uendeshaji wa mashauri ya kijinai.

"Tunalo jukumu la kupambana na uhalifu, na sisi ndio kiungo katika mapambano hayo, kwa hiyo tupambane vizuri ili Watanzania waweze kuishi kwa amani, kwani pasipokuwa na amani wala usalama,hakuna maendeleo katika Taifa letu. Hivyo tukiwa kama viongozi yatupasa kutekeleza Dira na Dhima iliyotolewa na Taasisi yetu"

Ameyasema hayo Mkurugenzi wa Mashtaka wakati akifungua Kikao kazi cha Wakuu wa Mashtaka Mikoa na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kilichofanyika tarehe 12 hadi 13 Mei, 2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mwakitalu alieleza kuwa katika siku hizi za karibuni kumekuwa na ongezeko la wimbi la uhalifu katika nyanja zote. Hivyo basi kuna jukumu kubwa la kulinda haki hususani zile ambazo zinaangukia kwenye jinai.

DPP aliwapongezaWakuu wa Mashtaka Mikoa kwackufanya kazi nzuri ya kupunguza msongamano wa mahabusu gerezani ijapokuwa bado changamoto hiyo ya msongamano haijaisha.

"Magereza yaliyomengi khali sio nzuri lakini kibaya zaidi Mahabusu ni wengi kuliko wafungwa. Kwahiyo kupitia hili inabidi kujadili kwa kina ili kuweza kupata suluhu ya kupunguza mlundikano mkubwa wa mashauri yaliyopo mahakamani"

Aidha Mwakitalu alisema kuwa ni muhimu kupata taarifa za kila siku kwani zitasaidia kupanga mipango ya maendeleo ya kiofisi. Na pia aliendelea kueleza kuwa kwa upande wa eneo la Takwimu ni muhimu kuangaliwa kwa umakini zaidi ili ziweze kuendana na uhalisia hususani katika eneo la Takwimu za Mahakama za Mwanzo kwasababu zinalenga kesi za jinai. Hivyo basi ni muhimu kuwa na taarifa zake ili kuona idadi ya kesi zilizosajiliwa, zilizoisha, na kujua zimeishaje na faini kiasi gani. Hivyo ni eneo muhimu sana sana la kuangaliwa na kupata ufumbuzi wake.

Naye pia Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande alielezakuwalengo kuu la kufanya kikao kazi hicho ni kufanya tathmini ya ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, hivyo basikikao hicho kimepanga kutoka namaadhimio juu ya namna gani ifanyike ili kukabiliana na ongezeko la uhalifu na pia kutengeneza mikakati ya pamoja ya namna ya kukabiliana na kesi za jinai ili kuweza kudumisha haki na amani katika Taifa la Tanzania.