Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kupatikana na madawa ya kulevya
18 Sep, 2020
Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kupatikana na madawa ya kulevya

Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam mbele ya Mhe. Jaji Mashaka imemuhukumu kifungo cha miaka thelathini jela Said Shaban Malikita kwa kosa la kupatikana na madawa ya kulevya aina ya Heroin hydrochloride yenye gramu 238.24.

Mshtakiwa Said Shaban Malikita alikamatwa na madawa hayo tarehe 29/8/2017 eneo la mtaa wa Ufipa Kinondoni.

Katika shauri hilo upande wa Mashtaka ukiwakilishwa na Mawakili wa Serikali Costantine Kakula na Batilda uliwasilisha mashahidi nane na vielelezo vitano ili kudhibitisha kesi.

Baada ya kuchambuliwa kwa ushahidi kwa ujumla wake upande wa Mahakama uliona kwamba upande wa Jamhuri umedhibitisha kesi bila kuacha shaka na hivyo kumuhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka thelathini jela.

Katika kesi hiyo Mawakili wa Serikali uliwakilishwa na Mawakili Costantine Kakula na Batilda Mushi na upande wa utetezi uliwakilishwa na Abraham Senguji.