Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la ubakaji
27 Aug, 2020
Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la ubakaji

Mahakama ya Wilaya ya Babati leo tarehe 27/08/2020 imemtia hatiani SAID JUMA @Rasii miaka 36 ,mkazi wa kijiji cha Kisangaji Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka minne(jina limehifadiwa),na kumuhukumu kutumikia kifungo cha maisha jela kitendo hicho ni kinyume namba 130(1),(2)(e) na 131(1),(3) vya kanununi ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo. Mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 8/03/2020 katika kijiji cha Kisangaji Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali Luciana Shabani uliwasilisha mahakamani mashahidi watano huku upande wa utetezi ukiwa na shaidi mmoja pekee. Shauri hilo la jinai 70/2020 lilisajiliwa mahakamani hapo mnamo tarehe 1/04/2020 mbele ya muheshiwa Victor Kimario, Hakimu Mkazi Mwandamizi na Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Babati.