Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

WAOMBOLEZAJI MBALIMBALI WASHIRIKI KUAGA MWILI WA PETER MAUGGO
26 Oct, 2024
WAOMBOLEZAJI MBALIMBALI WASHIRIKI KUAGA MWILI WA PETER MAUGGO

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi tarehe 22 Oktoba, 2024 ameshiriki kwenye ibada ya kumuaga aliyekuwa Mfanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka marehemu  Peter Mauggo iliyofanyika nyumbani kwake Ilazo  Jijini Dodoma.

Akizungumza na waombelezaji Waziri Kabudi alisema  watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wanapaswa kuyaenzi mazuri yote yaliyofanywa na marehemu wakati wa uhai wake yakiwepo masuala ya kuzingatia  weledi, nidhamu pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta chachu ya maendeleo katika taifa letu.

Katika tukio hilo, Waziri Kabudi aliwasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alitoa pole kwa watumishi wote wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka pamoja na familia kwa ujumla kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Viongozi wengine walioshiriki katika ibada ya maombolezo hayo ni Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi ,Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Eleuter Kihwele na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula.