Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

MASHTAKA SACCOS YAZINDULIWA RASMI
16 Apr, 2023
MASHTAKA SACCOS YAZINDULIWA RASMI

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester  Mwakitalu amezindua rasmi Chama cha Akiba na Mikopo cha Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (Mashtaka SACCOS).

Akizindua SACCOS hiyo mapema leo  tarehe 6 Aprili, 2023 kwenye kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kilichofanyika mjini Morogoro Bw. Mwakitalu amesema Saccos hiyo itakuwa msaada mkubwa wa utatuzi wa changamoto  za wafanyakazi.

Mwakitalu ameongeza kuwa ni wakati wa watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuitumia kuboresha na kuimairisha maisha yao kupitia SACCOS hiyo ambayo imeasisiwa katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Sambamba na hayo Mkurugenzi wa Mashtaka amewataka watumishi ambao bado hawajajiunga na Mashtaka SACCOS waweze kujiunga kwani itasaidia katika kutatua changamoto za kifedha kwa watumishi hao.

Nao baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wamepongeza hatua hiyo ya kuzinduliwa kwa Mashtaka SACCOS ambayo itakuwa msaada kwao kwa kuwa wataitumia kuinua uchumi wao na kubadili maisha yao.