Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

KAIMU MKURUGENZI KWEKA AMESISITIZA MATUMIZI YA MFUMO KATIKA UPANDE WA TAKWIMU
08 Jan, 2022
KAIMU MKURUGENZI KWEKA AMESISITIZA MATUMIZI YA MFUMO KATIKA UPANDE WA TAKWIMU

Kaimu Mkurugenzi Divisheni ya Utenganishaji wa Shughuli za Mashtaka na Upelelezi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma amewataka Makatibu Sheria na Mawakili kutumia nafasi hii ya mafunzo, kujifunza namna ya kuutumia mfumo huu vizuri ili kuwasaidia katika kazi zao mbalimbali za kila siku hususani kwa upande wa Takwimu ambapo kwa kupitia mfumo huu utasaidia kuingiza taarifa zilizo sahihi.

Aidha, alieleza kuwa kwa kupitia Takwimu zilizopo kwenye mfumo zitatoa majibu ya mahitaji yote ya kiofisi na pia itawasaidia Mawakili pamoja na Makatibu Sheria kujua ni idadi ngapi za kesi zilizopokelewa kutoka nchi nzima.

"Roho ya Taasisi yoyote ni Takwimu kwani ndio roho ya nchi. Ni wajibu wenu kuhakikisha kwamba huu mfumo mnauelewa vizuri na kuutunza."

Amezungumza hayo Mkurugenzi Kweka wakati akifanya ufunguzi wa awamu ya pili ya Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielekitroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya Kesi kwa Makatibu Sheria na baadhi ya Mawakili wa Serikali wanaoshughulika na Takwimu yaliyoanza mnamo tarehe 5 Januari 2022 na kumalizika tarehe 8 Januari, 2022 Jijini Dar es salaam katika ofisi za TAGLA zilizopo Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM)