Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

MKURUGENZI KWEKA AWATAKA WAENDESHA MASHTAKA NA WADAU KUHAKIKISHA HAKI ZA WATOTO ZINALINDWA
21 Jul, 2023
MKURUGENZI KWEKA AWATAKA WAENDESHA MASHTAKA NA WADAU KUHAKIKISHA HAKI ZA WATOTO ZINALINDWA

"Tuutumie ule weledi tulionao katika kuhakikisha Haki za Watoto  wanaokinzana na wanaohusishwa na Sheria zinalindwa" - Mkurugenzi Kweka 

Mkurugenzi wa Divisheni ya Utenganishaji wa Shughuli za Mashtaka na Upelelezi Bw. Tumaini Kweka amewataka Waendesha Mashtaka na Wadau kutoka Taasisi mbalimbali kuhakikisha wanatoa michango yao kwa usahihi katika kuboresha Rasimu ya Mwongozo wa Uendeshaji wa Kesi za Watoto kwa lengo la kulinda haki zao.
 
Mkurugenzi Kweka amebainisha hayo wakati akifungua Kikao kazi cha Wadau kwa ajili ya kutoa maoni ya kuboresha Rasimu ya Mwongozo wa Uendeshaji wa Kesi za Watoto kwa Waendesha Mashtaka kinachofanyika Jijini Dodoma kuanzia tarehe 20 hadi 21 Julai, 2023.

Aidha, Mkurugenzi Kweka ameeleza kuwa, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha wanawalinda na kuwajenga Watoto kuwa  raia bora hapo badae  hivyo Waendesha Mashtaka na Wadau wanapaswa kuboresha Rasimu ya Mwongozo wa Uendeshaji wa Kesi za Watoto  kulingana na mahitaji husika zikiwemo changamoto na mapungufu katika uendeshaji wa kesi hizo.