Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 ARINSA JIJINI DAR ES SALAAM
28 Aug, 2019
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 ARINSA JIJINI DAR ES SALAAM

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 ARINSA JIJINI DAR ES SALAAM

Makamau wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassam ameuhakikishia Mtandao wa kupambana na uhalifu kwa njia ya utaifshaji wa mali zinazohusiana na Uhalifu kwa nchi za KusinI mwa Afrika (ARINSA) kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuunga mkono kwa dhati juhudi za Nchi wanachama wa umoja huo katika kufikia malengo yake ili kuhakikisha kuwa nchi za ukanda huo zinakuwa salama, kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wake.

Mhe. Samia alikuwa akizundua maadhimisho ya miaka 10 ya umoja huo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amezitaka nchi wanachama kuheshimu na kutekeleza tamko la pamoja la Dar es Salaam (The Dar es Salaam Declaration) lenye kuashiria nia ya pamoja ya kupambana na uhalifu kwa njia ya utaifshaji wa mali zinazohusiana na Uhalifu huku akiziagiza ARINSA na NPS kutafuta suluhisho la changamoto zilizopo ili umoja huo uwe wa manufaa zaidi.


Amewataka NPS na ARINSA kuangalia namna ya kukamilisha wazo la kujenga Taasisi Mahsusi kwa ajili ya kuwajengea uwezo waendesha mashtaka wapya na waliopo kazini kwakuwa kuanzishwa kwa taasisi hiyo kupunguza gharama zinazotumiwa na umoja na hivyo kuleta matokeo chanya kwa kazi nzuri iliyoanzishwa na ARINSA.


Ametaka idadi ya wapelelezi na waendesha mashataka iongezeke ili waendane na wingi wa mashauri yanayohusiana na utaifishaji na urejeshaji wa mali zinazohusiana na uhalifu na kuongeza kuwa Wapelelezi na waendesha mashtaka wajengewa uwezo zaidi katika kupeleleza na kuendesha mashtaka katika makosa ya kifedha (Financial Crimes), wanyamapori, misitu na ufadhili wa ugaidi ikiwa ni pamoja na kufuatilia mali walizozipata wahalifu hao au walizozitumia kutendea uhalifu ili kuzitaifisha.


Ampongeza Bw. Biswalo Mganga kwa kuwa Rais wa ARINSA kwa kuaminiwa kwake ni chachu ya kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu hapa nchini na Afrika kwa ujumla kwa kuhalkikisha kuwa wahalifu hawafaidiki na mali zitokanazo na uhalifu.

Maadhimisho na mkutano huo wa mwaka umehudhuriwa na wanachama wa Umoja huo kutoka nchi za Angola, Botswana, Eswatini, Kenya, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania.