Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

DPP ASISITIZA JUU YA MATUMIZI YA MFUMO KWA MAKATIBU SHERIA NA WATUNZA KUMBUKUMBU.
01 Mar, 2024
DPP ASISITIZA JUU YA MATUMIZI YA MFUMO KWA MAKATIBU SHERIA NA WATUNZA KUMBUKUMBU.

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amewasisitiza Makatibu Sheria pamoja na Watunza Kumbukumbu kuusimamia na kuutumia Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya, Kuchakata na Kutunza Kumbukumbu za Kesi za Jinai (Case Management Information System) kwa lengo la kuweza kuwasaidia kupata takwimu zilizo sahihi za kesi zitakazosaidia katika kufanya maamuzi na kupanga mipango ya maendeleo. 

Mkurugenzi Mwakitalu amebainisha hayo wakati akifungua Kikao kazi cha Mkurugenzi wa Mashtaka na Makatibu Sheria pamoja na Watunza Kumbukumbu kinachofanyika tarehe 29 Februari, 2024 hadi 1 Machi, 2024 Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mashtaka amesema kuwa kikao kazi hicho kimelenga kufahamiana, kubadilishana mawazo na kukumbushana majukumu yao kupitia mada mbalimbali zitakazowasilishwa na Wawezeshaji.

Aidha Mkurugenzi wa Mashtaka amewataka washiriki hao kutumia fulsa hiyo kujadiliana na kutafuta suluhu ya changamoto ambazo wanakabiliana nazo wakati wa utendaji kazi wao  ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Tunataka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iwe ni ofisi bora zaidi katika maeneo yote ya kiutendaji hususani katika Usimamizi na Uendeshaji wa Kesi. Kila mmoja atekeleze majukumu yake kwa uadilifu, bidii nakwa nguvu zake zote." Ameyasema hayo Mkurugenzi Mwakitalu.