Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Muundo wa Ofisi
 1. UTANGULIZI

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeanzishwa kama Ofisi huru ya Umma kupitia Tangazo la Serikali Na.49 la mwaka 2018 la tarehe 13 Februari, 2018 la kuanzisha Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya kutekeleza mamlaka ya Kikatiba aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka ambaye anatoa mchango mkubwa katika kusimamia haki jinai.   Kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Mkurugenzi wa Mashtaka amepewa uwezo na mamlaka ya kusimamia uendeshaji wa mashtaka yote ya jinai katika Mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi.   Kwa msingi huo, Mkurugenzi wa Mashtaka ana uwezo wa kufungua, kuendesha na kusimamia mashtaka yote ya jinai nchini.   Kutokana na Ibara hiyo ya Katiba, Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka hayamhusu mtu mwingine yoyote au mamlaka nyingine na hawajibiki kusimamiwa na mtu mwingine yoyote au mamlaka nyingine.   Katika kutekeleza majukumu yake, Mkurugenzi wa Mashtaka anatakiwa kufuata kanuni zifuatazo:  Kutenda haki; Kuzuia ukiukaji wa taratibu za kisheria; na maslahi ya umma.   Nafasi hii imewekwa chini ya kifungu cha 8 cha Sheria ya Taifa ya Mashtaka, Sura ya 430.

Tangazo la Serikali Na.49 la mwaka 2018 limeweka mpangilio wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, muundo wake, utawala, ufuatiliaji usimamizi wa mashtaka na namna uratibu wa upelelezi utakavyokuwa kwa lengo la kukuza na kuinua utendaji haki jinai na masuala yanayohusiana nayo.

 1. DIRA NA DHIMA

1.1.1   DIRA

Haki, amani na usalama kwa maendeleo ya Taifa.

1.1.2   DHIMA

Kushirikiana na wadau na kuendesha kesi bila woga, upendeleo ili kuhakikisha uwepo wa   haki, amani, na usalama katika jamii.

1.2     MAADILI YA MSINGI

Maadili ya Msingi ni-

 1. Uwajibikaji:  Kuwajibika  katika utekelezaji wa majukumu  kwa wakati;
 2. Kukubalika:  Uthabiti na uwezo wa kuaminika na kuthaminiwa;
 3. Uadilifu: Kwa maadili na uaminifu bila kuvumilia vitendo vya rushwa na ubadhirifu;
 4. Uweledi:  Kwa kujituma, kujitoa, umahili na utaalamu ndani na nje ya ofisi;
 5. Huduma bora: Kwa kutoa huduma bora kwa kufanya kazi pamoja, heshima na adabu.

1.3     SABABU ZA MUUNDO ULIOPENDEKEZWA

Sababu zilizopelekea kupendekezwa Muundo hu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni utekelezaji wa mfumo ulioainishwa katika Ibara ya 59B(3) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sheria ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Sura 430 na Amri ya Kuanzisha Muundo wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, (Tangazo la Serikali Na.49 la mwaka 2018).

2.0     MUUNDO ULIOPITISHWA

Muundo ulipitishwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unajumuisha Divisheni Sita (6) na Vitengo Saba (7) kama ifuatavyo:

 1. Divisheni ya Kusimamia Uendeshaji Mashtaka;
 2. Divisheni ya Utaifishaji Mali, Makosa yanayovuka Mipaka na Uhalifu Mahsusi;
 3. Divisheni ya Usimamizi wa Kesi;
 4. Divisheni ya Makosa ya Udanganyifu, Utakatishaji Fedha na Rushwa;
 5. Divisheni ya Utawala na Rasilimali Watu;
 6. Divisheni ya Mipango

vii) Kitengo cha Huduma ya Utafiti na Maktaba;

(viii)Kitengo cha Masjala ya Sheria;

(ix)Kitengo cha Ununuzi na Ugavi;

(x)Kitengo cha Uhasibu na Fedha;

(xi)Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani;

(xiii)Kitengo cha TEHAMA;

(xiv)Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

2.1     MAJUKUMU NA WAJIBU

2.1.1   MKURUGENZI WA MASHTAKA

Mkurugenzi wa Mashtaka ni mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Mkurugenzi wa Mashtaka ndiye msimamizi mkuu wa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Mawakili wa serikali na Waendesha Mashtaka katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka yatakuwa ni:

 1. Kuamua kushtaki au kutoshtaki kwenye makosa ya jinai;
 2. Kuanzisha, kuendesha na kusimamia mashtaka ya makosa ya jinai katika mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi;
 3. Kutwaa na kuendelea na mashtaka ya kesi yoyote ya jinai iliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine;
 4. Kufuta mahakamani mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine katika hatua yoyote kabla hukumu kutolewa;
 5. Kutoa maagizo kwa jeshi la polisi au vyombo chunguzi vyoyote kuchunguza taarifa yoyote ya kijinai na kutoa taarifa kwake haraka inavyowezekana;
 6. Kuchukua hatua muhimu kwa jambo lolote lenye tija katika mashtaka ya jinai;
 7. Kutoa miongozo inayohusu uratibu wa upelelezi na uendeshaji mashtaka;
 8. Kuteua na kutengua mamlaka ya waendesha mashtaka wa umma;
 9. Kumshauri waziri mwenye dhamana katika masuala ya mashtaka yanayohitaji sera au hatua za kibunge;
 10. Kuteuwa maafisa maalum ndani ya taasisi za serikali kusimamia mali zilizozuiliwa au kutaifishwa na mahakama katika mazingira ambayo ni vigumu kuteua wasii;
 11. Kufanya kazi nyingine ambayo zinahusiana na mashtaka ya umma;
 12. Kuwasimamia maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine walioteuliwa au kuajiriwa na ofisi ya taifa ya mashtaka;
 13. Kusimamia shughuli zote zinazofanywa na maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka;
 14. Kuita afisa yoyote wa umma kutoa maelezo au taarifa kuhusiana na jambo lolote ambalo linahusu mashtaka ya umma;
 15. Kuandaa na kuwasilisha kwa waziri taarifa ya nusu mwaka na nakala kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya taifa ya mashtaka; na
 16. Kuteua au kuajiri na kuwajibisha maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka.

2.1.1.1          NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Mkurugenzi wa Mashtaka na atafanya majukumu yake kadri atakavyoelekezwa na Mkurugenzi wa Mashtaka. Aidha Naibu Mkurugenzi wa mashtaka atakuwa ndiye afisa masuuli wa taasisi na atasimamia shughuli za kila siku za taasisi na atakuwa mamlaka ya nidhamu ya watumishi kwa mujibu wa kanuni na sheria za utumishi wa umma. Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ataandaa kanuni za nidhamu kwa waendesha mashtaka na kuhakikisha viwango vya kimataifa vinazingatiwa na ndiye atatunza kumbukumbu za waendesha mashtaka wa umma.

2.1.1.1.1        DIVISHENI YA KUSIMAMIA UENDESHAJI MASHTAKA.

Lengo: kutoa ushauri wa kitaalamu na huduma za uendeshaji mashtaka nchini.

Majukumu:

Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 1. Kuratibu utekelezaji wa programu ya uendeshaji wa mashtaka;
 2. Kuratibu na kuandaa miongozo inayohusu upelelezi na uendeshaji kesi za jinai;
 3. Kusimamia ukaguzi, ufatiliaji na ubora wa huduma zinazotolewa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka;
 4. Kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa miongozo inayotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka kuhusiana na upelelezi na uendeshaji mashtaka ya jinai;
 5. Kuratibu upelelezi ili kuhakikisha ufanisi katika upelelezi unaoratibiwaa na mwendesha mashtaka
 6. Kuratibu na kusimamia matumizi bora ya mwongozo wa waendesha Mashtaka na Mwongozo wa Wapelelezi;
 7. Kuandaa mahitaji ya mafunzo ya kisheria ili kuleta tija katika mashtaka;
 8. Kuratibu ukaguzi wa sero za polisi na magereza;
 9. Kuratibu ufuatiliaji wa majukumu waliyopangiwa kwa watumishi na maafisa wengine ndani ya taasisi;
 10. Kutafuta ufumbuzi wa masuala ya kisheria yanayotokana na maamuzi ya mahakama ambayo yanahitaji utekelezaji wa wadau wengine;
 11.      Kushirikisha wadau   wa haki jinai katika   masuala ya kesi za jinai;
 12. Kuratibu ukusanyaji wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kuhusiana na kesi zinazoendelea au kuisha   ili kuleta tija katika uendeshaji wa kesi za jinai;
 13. Kuratibu uchambuzi wa taarifa zilizokusanywa;
 14. Kuratibu ukusanyaji taarifa za mashauri ya jinai, kuchambua kitakwimu ili kupata taarifa zitakazosaidia kuleta tija katika mashtaka na hivyo kupunguza makosa ya jinai;
 15. Kufungua   kuendesha na kusimamia   mashtaka na
 16. Kusimamia rufaa na maombi ya jinai mahakamani kwa niaba ya Jamhuri.

Divisheni hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na sehemu tatu (3) zifuatazo:

 1. Sehemu ya uendeshaji mashtaka;
 2. Sehemu ya usimamizi wa   mashtaka mahakamani; na
 3. Sehemu ya makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa Taifa.

2.1.1.1.1.1 Sehemu ya Uendeshaji mashtaka

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 1. Kuratibu utekelezaji wa programu ya uendeshaji mashtaka;
 2. Kuandaa miongozo ya uendeshaji   wa mashtaka;
 3. Kufuatilia na kutathimini   utekelezaji wa miongozo inayotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka kuhusiana na upelelezi na uendeshaji mashtaka ya jinai;
 4. Kuandaa na kutunza kanzi data ya waendesha mashtaka na mawakili wa serikali;
 5. Kuratibu na kusimamia mipango na upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya programu ya uendeshaji mashtaka;
 6. Kuratibu   utwaaji wa uendeshaji mashtaka toka vyombo chunguzi   nchini;
 7. Kuhabarisha umma kuhusu masuala ya uendeshaji mashtaka;
 8. Kuratibu na kushauri sera, sheria, kanuni, miongozo na viwango katika kushughulikia makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 9. Kuratibu kesi zinazohusiana na makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 10. Kuratibu utekelezaji wa sheria katika vyombo vinavyotekeleza sheria vinavyohusu makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 11. Kuratibu ushirikiano wa kitaifa, kimataifa na kikanda na wadau wengine katika mapambano dhidi ya makosa ya binadamu na utengamano wa taifa na
 12. Kuratibu masuala yanayohusiana na mkanganyiko wa   sheria   za ukatili wa kijinsia na   watoto.

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

2.1.1.1.1.2 Sehemu ya Menejimenti ya Mashtaka

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 1. Kufuatilia, kukusanya na kuchambua taarifa za kesi zinazoendelea na zilizoisha ili kuelewa muundo na tabia za kesi;
 2. Kukusanya na kuchambua taarifa za kesi za wakosaji wa pekee na washirika wao kwa lengo la kusimamia na kupata taarifa za kiintelejensia zitakazowezesha uendeshaji bora wa mashtaka nchini;
 3. Kuratibu ukusanyaji taarifa za mashauri ya jinai, kuzichambua kitakwimu ili kupata taarifa zitakazosaidia kuleta tija katika uendeshaji wa   mashtaka;
 4. Kuanzisha na kutunza kanzi data ya taarifa za kiintelejensia;
 5. Kuwezesha ubadilishanaji wa taarifa za kiintelijensia na maafisa wanaoshughulikia kesi   ili kuweza kuandaa mfumo wa   kieletroniki wa   kesi (casedocket) na uendeshaji wake   mahakamani; na
 6. Kuwezesha ubadilishanaji wa taarifa za kiintelijensia na wadau wengine ili kupunguza uhalifu na hivyo kudumisha amani na usalama wa nchi

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

2.1.1.1.1.3     Sehemu ya makosa dhidi ya Binadamu na Utengamano wa Taifa.

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 1. Kupitia na kushauri kuhusu sera, sharia, kanuni, miongozo na viwango katika kusimamia mashauri ya makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 2. Kusimamia   kesi dhidi ya binadamu na utengamano wa kitaifa;
 3. Kusimamia vyombo vinavyotekeleza sheria katika mapambano dhidi ya makosa ya binadamu na utengamano wa taifa;
 4. Kufuatilia   uanzishaji na uendeshaji wa kesi za makosa   dhidi ya binadamu   na utengamano wa taifa na yanayohusiana na hayo katika ngazi ya mkoa na wilaya;
 5. Kufungua na kuendesha kesi za makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa kitaifa na yanayohusiana nayo;
 6. Kusimamia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za   makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 7. Kusimamia mapitio ya majalada yanayohusiana na makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 8. Kuwasiliana na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikanda pamoja na wadau wengine katika mapambano   ya makosa   dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 9. Kusimamia chunguzi za vifo vya mashaka;
 10. Kushauri kuhusu namna bora ya kutunza amani, usalama na utulivu wa nchi;
 11. Kushughulikia masuala yote yanayohusu mkanganyiko wa sheria dhidi ya ukatili wa jinsia na watoto.
 12. Kusimamia rufaa na maombi mbalimbali mahakamani yanayohusu makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa; na.
 13. Kushughulikia rufaa na maombi mbalimbali ya kesi za makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa.

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

2.1.1.1.2       DIVISHENI YA UTAIFISHAJI MALI, MAKOSA YANAYOVUKA MIPAKA NA UHALIFU MAHSUSI

Lengo: kutoa utaalamu na huduma ya kunyang’anya wahalifu au washirika wao faida zitokanazo na vitendo vya uhalifu pamoja na kuendesha kesi hizo mahakamani.   

Majukumu

Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 1. Kuratibu utekelezaji wa sheria pamoja na masuala yote yahusuyo utaifishaji na urejeshaji   mali zitokanazo na uhalifu;
 2. Kufuatilia na kusimamia ufunguaji na uendeshaji wa kesi zinazohusiana na utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika kutenda uhalifu na mazalia yake;  
 3. Kuratibu tathmini ya ufanisi wa sheria, kanuni, miongozo na viwango kwenye masuala ya utaifishaji na urejeshaji mali zitokanazo na uhalifu na kupendekeza marekebisho yake;
 4. Kuratibu utambuzi na ufuatiliaji wa zana zinazotumika katika kutenda uhalifu   na mazalia yake;
 5. Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kimataifa na kikanda katika ufuatiliaji, utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika katika kutenda uhalifu na mazalia yake;
 6. Kufuatilia na kusimamia utambuzi wa kesi zenye uwezekano wa kuwa na mali za kurejesha;
 7. Kufuatilia na kusimamia mali zilizozuiliwa, taifishwa na kurejeshwa;
 8. Kutoa ushauri na muongozo kuhusu maombi ya utaifishaji na urejeshaji wa mali zinazotumika katika kutenda uhalifu na mazalia yake, yanayoombwa kwa au na    jamhuri ya muungano wa tanzania;
 9. Kuratibu, kutathimini na kushauri ufanisi wa sera, sheria, kanuni, miongozo na viwango vya usimamizi wa makosa yanayovuka mipaka na kupangwa;
 10. Kuratibu na kutoa miongozo kwa mamlaka zinazotekeleza sheria katika masuala yahusuyo makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa;
 11. Kufuatilia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za makosa yanayovuka mipaka na kupangwa katika ngazi za   mikoa na wilaya;
 12. Kufungua na kuendesha kesi za makosa yanayovuka mipaka, ya kupangwa na masuala yanayohusiana nayo;
 13. Kusimamia mapitio ya majalada yanayohusiana na makosa yanayovuka mipaka   na ya kupangwa toka vyombo chunguzi;
 14. Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikanda   pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa;
 15. Kuratibu na kusimamia masuala yanayohusu ubadilishanaji wa wahalifu watoro kama itakavyoelekezwa na waziri mwenye dhamana na masuala ya sheria;
 16. Kushauri kwenye masuala ya ushirikiano wa kesi za jinai;
 17. Kusimamia uendeshaji wa kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa;
 18. Kuwezesha uhudhuriaji wa mashahidi kutoka na kwenda nje ya nchi kutoa ushahidi;
 19. Kuratibu na kutoa miongozo kwa mamlaka zinazotekeleza sheria katika masuala ya makosa ya kimtandao;
 20. Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikanda   pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya makosa ya kimtandao; na
 21. Kuratibu na kushauri ufanisi katika uendeshaji wa kesi za makosa ya kimtandao.

Divisheni hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na Sehemu tatu (3) kama ifuatavyo:

 1. Sehemu ya utaifishaji na urejeshaji   mali;
 2. Sehemu ya Makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa; na
 3. Sehemu ya Makosa ya kimtandao.

2.1.1.1.2.1    Sehemu ya Utaifishaji na Urejeshaji Mali

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 1. Kusimamia utekelezaji wa Sheria za utaifishaji na urejeshaji mali pamoja   na masuala mengine yanayohusiana nayo;
 2. Kutathmini na kushauri ufanisi wa Sheria, Kanuni, Miongozo na viwango kwenye masuala ya utaifishaji na urejeshaji mali zitokanazo na uhalifu na kupendekeza marekebisho yake;
 3. Kusimamia utambuzi wa kesi zenye uwezekano wa kuwa na mali za kurejesha;
 4. Kufungua na kuendesha kesi zinazohusu utaifishaji   na urejeshaji   mali ndani na nje ya   nchi;
 5. Kusimamia utambuzi na ufuatiliaji wa zana zinazotumika katika kutenda uhalifu na mazalia yake;
 6. Kushirikiana na mashirika ya kimataifa na kikanda katika ufuatiliaji, utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika katika kutenda uhalifu na mazalia yake;
 7. Kusimamia utekelezaji wa sheria za utaifishaji na urejeshaji   mali pamoja masuala yanayohusiana nayo;
 8. Kutathmini na kushauri kuhusiana na ufanisi wa sheria, Kanuni, Miongozo na viwango katika utekelezaji wa amri za utaifishaji na urejeshaji mali na kupendekeza marekebisho;
 9. Kusimamia utekelezaji wa amri za uzuiaji na utaifishaji mali pamoja na wadau wa urejeshaji mali; 
 10. Kushirikiana na mashirika ya kimataifa na kikanda katika utekelezaji wa amri za utaifishaji na urejeshaji mali;
 11. Kusimamia   mali zilizozuiliwa, taifishwa na kurejeshwa;
 12. Kushauri juu ya uondoshaji na ugawanyaji wa mali zilizotaifishwa;
 13. Kuandaa   na kutunza kumbukumbu za mali zote zilizo shikiliwa, zuiliwa, taifishwa na kurejeshwa; na
 14. Kutathmini mali zilizozuiliwa, taifishwa na kurejeshwa kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali.

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

2.1.1.1.2.2    Sehemu ya Makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 1. Kutathmini na kushauri kuhusiana na ufanisi wa Sera, Sheria, Kanuni,Miongozo na viwango katika usimamizi wa kesi za madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia na kupendekeza marekebisho;
 2. Kuwasiliana na taasisi zinazotekeleza Sheria kwenye masuala yanayohusiana na makosa ya madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia;
 3. Kufuatilia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia pamoja na masuala yanayohusiana nayo katika ngazi za mikoa na wilaya;
 4. Kufungua na kuendesha kesi za makosa ya madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia pamoja na masuala yanayohusiana nayo.
 5. Kusimamia na kushauri uendeshaji wa kesi za   madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia ili kuleta tija;
 6. Kufanya mapitio ya majalada toka vyombo chunguzi na kutoa maelekezo stahiki kuhusiana na makosa ya madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia;
 7. Kutoa ushauri na maoni ya kisheria kwa taasisi za kimataifa na mamlaka zinazoshughulikia   makosa ya madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia;
 8. Kutathmini na kushauri ufanisi wa Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na Viwango katika usimamizi wa   makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikiano katika kesi za jinai   na kupendekeza marekebisho;
 9. Kuwasiliana na taasisi nyingine zinazotekeleza sheria katika masuala yanayohusiana na usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikiano katika kesi za   jinai kulingana na Sheria na taratibu husika;
 10. Kufungua na kuendesha kesi zinazohusiana na usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikiano katika kesi za jinai kulingana na Sheria na taratibu husika;
 11. Kusimamia na kushauri   uendeshaji wa kesi za usafirishaji haramu wa binadamu ili kuleta tija;
 12. Kufanya mapitio ya majalada toka vyombo chunguzi na kutoa maelekezo stahiki kuhusiana na makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikiano katika kesi za jinai;
 13. Kuwasiliana na taasisi za kitaifa, kimataifa na kikanda pamoja na wadau katika masuala ya usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikiano   katika kesi za jinai;
 14. Kutoa ushauri na maoni ya kisheria kwa taasisi za kimataifa na mamlaka zinazoshughulikia makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikiano katika kesi za jinai;
 15. Kushughulikia na kushauri kuhusu ushirikiano katika kesi za jinai pale ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaomba au inaombwa na mamlaka za nchi nyingine.
 16. Kushughulikia masuala yanayohusiana na wahalifu watoro, uhamishaji wa wafungwa na kutafuta mashahidi; na
 17. Kushughulikia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na utwaaji wa wahalifu
 18. Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

2.1.1.1.2.3    Sehemu ya Makosa ya Kimtandao

Sehemu hii itafanya kazi zifuatazo:

 1. Kutathmini na kutoa ushauri   kuhusiana na ufanisi wa   Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na viwango katika usimamizi wa makosa ya kimtandao na kupendekeza marekebisho;
 2. Kuwasiliana na taasisi zinazotekeleza sheria za makosa ya kimtandao na yale yanayohusiana nayo;
 3. Kufuatilia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za makosa ya kimtandao katika ngazi ya mikoa na wilaya;
 4. Kufungua   na kuendesha kesi za makosa ya kimtandao;
 5. Kusimamia na kutoa   ushauri wa uendeshaji wa kesi za makosa ya kimtandao kwa ufanisi;
 6. Kufanya mapitio ya majalada toka vyombo chunguzi na kutoa maelekezo stahiki kuhusiana na makosa ya kimtandao;
 7. Kuwasiliana na taasisi za kitaifa, kimataifa na kikanda pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya makosa ya kimtandao; kna
 8. Kushughulikia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na makosa ya   kimtandao.
 9. Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

   2.1.1.1.3      DIVISHENI YA MAKOSA YA UDANGANYIFU, UTAKATISHAJI FEDHA NA RUSHWA

  Lengo: Kutoa utaalamu na huduma ya mashtaka kwa makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha, rushwa, mazingira na mali asili.

  Majukumu

Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 1. Kupitia na kutoa ushauri kwenye sera. Sheria, kanuni, miongozo na viwango katika usimamizi wa makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha   na rushwa;
 2. Kuratibu kesi za rushwa katika mahakama kuu kitengo cha makosa ya rushwa na uhujumu uchumi   na mahakama za chini;
 3. Kuratibu taasisi zinazotekeleza sheria katika   makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha, rushwa na masuala yanayohusiana nayo;
 4. Kusimamia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za udanganyifu na rushwa katika ngazi za mikoa na wilaya;
 5. Kufungua na kuendesha kesi za rushwa na udanganyifu;
 6. Kusimamia mapitio ya majalada ya kesi za utakatishaji fedha, rushwa na udanganyifu;
 7. Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikanda pamoja na   wadau katika kupambana na   makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha na rushwa;
 8. Kusimamia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha na rushwa; na
 9. Kushughulikia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na rushwa na udanganyifu.

Divisheni   hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na sehemu (3) kama ifuatavyo:

 1. Sehemu ya makosa ya   udanganyifu na utakatishaji fedha;
 2. Sehemu ya makosa ya rushwa; na
 3. Sehemu ya mazingira na mali asili.

2.1.1.1.3.1    Sehemu ya makosa ya udanganyifu na utakatishaji fedha

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 1. Kutathmini na kushauri kuhusiana na ufanisi wa Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na viwango katika usimamizi wa kesi za udanganyifu na utakatishaji fedha na kupendekeza maboresho;
 2. Kuwasiliana na taasisi zinazotekeleza sheria katika masuala yanayohusiana na makosa ya udanganyifu na utakatishaji fedha na yanayohusiana nayo;
 3. Kufuatilia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za makosa ya udanganyifu na utakatishaji fedha katika ngazi za mikoa na wilaya;
 4. Kufungua na kuendesha kesi zinazohusiana na makosa ya rushwa na udanganyifu;
 5. Kusimamia na kushauri uendeshaji wa kesi za makosa ya udanganyifu na utakatishaji fedha ili kuleta tija;
 6. Kufanya mapitio ya majalada kutoka vyombo chunguzi na kutoa maelekezo stahiki kuhusiana na makosa   ya udanganyifu na utakatishaji fedha;
 7. Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikanda pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya makosa ya udanganyifu na utakatishaji fedha; na
 8. Kushughulikia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na makosa   ya udanganyifu na utakatishaji fedha

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

2.1.1.1.3.2    Sehemu ya Makosa ya Rushwa

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 1. Kutathmini na kushauri kuhusiana na ufanisi wa Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na viwango katika usimamizi wa kesi za rushwa na kupendekeza maboresho;
 2. Kuwasiliana na taasisi zinazotekeleza sheria za makosa ya rushwa na yanayohusiana nayo;
 3. Kusimamia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za rushwa na yanayohusiana nayo katika ngazi ya mkoa na wilaya;
 4. Kufungua na kuendesha kesi za rushwa na masuala yanayohusiana nayo;