Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

WAENDESHA MASHTAKA NA WAPELELEZI WAJENGEWA UWEZO
26 May, 2022
WAENDESHA MASHTAKA NA WAPELELEZI WAJENGEWA UWEZO

Serikali imeendelea kuwekeza katika kuwajengea uwezo Waendesha Mashtaka na Wapelelezi ili kuwawezesha kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya kimazingira na mbinu za kutenda makosa mbalimbali ya jinai yakiwepo ya Wanyamapori na Misitu.

Akifungua mafunzo ya Upelelezi na Uendeshaji wa kesi za Wanyamapori na Misitu kwa Wakuu wa Upelelezi na Waendesha Mashtaka nchini yanayofanyika mjini Moshi kuanzia tarehe 25 Mei, 2022, Kamishna Wambura alitoa rai kwa washiriki wa mafunzo kuhakikisha wanajiongezea maarifa yatakayowasaidia kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu alisema kuwa Wapelelezi na Waendesha Mashtaka ni wadau muhimu sana katika mnyororo wa Haki Jinai.

Aliendelea kueleza kuwa baada ya mafunzo anatarajia kuona mabadiliko makubwa katika utendaji wa kazi.

Aidha Mwakitalu alieleza kuwa ufanisi katika kesi unaanza toka matukio ya uhalifu yanapoanza na mnyororo wa ushirikiano huanzia hapo ambapo mnyororo ukikatika mahali matokeo tarajiwa sio rahisi kupatikana.

'' Changamoto za kiutendaji zinaanzia kwenye kufanya ukusanyaji ushahidi na utunzaji wa vielelezo hivyo mafunzo yanayotolewa yanalenga kutatua changamoto katika ngazi zote.

Aliyasema hayo Mkurugenzi wa Mashtaka Mwakitalu.

Naye pia Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande akizungumza katika mafunzo hayo alisema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imefanya operesheni maalum ya kusoma mafaili ambapo ni zaidi ya mafaili elfu moja mia saba na kufungua kesi elfu moja mia tatu na pia kesi zipatazo mia nne zimefutwa.

Naibu Mkurugenzi aliendelea kueleza kuwa ifikapo tarehe 16 Juni 2022, kesi zaidi ya Mia Mbili hamsini zitakuwa zimesomwa.

"Kesi hizi 250 zitasomwa ndani ya mwezi mmoja na zitasaidia kupunguza sana malalamiko yasiyo ya lazima kutoka kwa wananchi."

Alisema Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Joseph Pande