Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

Lengo: kutoa huduma za ushauri kwa Afisa wa Masuuli katika usimamizi sahihi wa rasilimali.

Kitengo hiki ktiakuwa na majukumu yafuatayo:

(i) Kufanya mapitio na kutoa ripoti kuhusu udhibiti katika upokeaji, utunzaji na matumizi ya rasilimali fedha;

(ii) Kufanya mapitio na kutoa ripoti juu ya uzingatiaji wa taratibu uendeshaji na kifedha kwa mujibu wa sheria , kanuni na maelekezo kwa ajili ya udhibiti wa matumizi;

(iii) Kufanya mapitio na kutoa ripoti juu ya usahihi wa uainishaji na ugawaji wa mapato na matumizi;

(iv) Kuandaa taratibu za ukaguzi ambazo hazikizani na viwango vya kimataifa;

(v) Kufanya mapitio na kutoa ripoti juu ya usahihi, uadilifu wa shughuli za kifedha, taarifa, kuandaa taarifa za kifedha na taarifa nyingine;

(vi) Kufanya mapitio na kutoa ripoti juu ya mfumo unaotumika kulinda mali na kuthibitisha uwepo wake;

(vii) Kufanya mapitio na kutoa ripoti juu ya uendeshaji au programu ili kuona kama matokeo yanaendana na madhumuni na malengo yaliyowekwa.

(viii) Kufanya mapitio na kutoa ripoti juu ya majibu yaliyotolewa na menejimenti kuhusu ripoti za ukaguzi wa ndani, na kusaidia menejimenti katika utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti na ufuatiliaji juu ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali;

(ix) Kufanya mapitio na kutoa ripoti juu ya utoshelevu wa udhibiti katika mifumo ya kompyuta.

(x) Kuandaa na kutekeleza mpango mkakati wa ukaguzi; na

(xi) Kufanya ukaguzi wa utendaji juu ya tathmini ya miradi ya maendeleo

Kitengo hiki kitaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani.