Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Divisheni ya Usimamizi wa Kesi

Lengo: kutoa utaalamu katika usimamizi wa kesi na uratibu wa upelelezi.

Majukumu:

Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

  • (i)Kutoa maelekezo katika usimamizi, ukaguzi na ufuatiliaji wa ubora katika uendeshaji wa huduma zinazotolewa na Ofisi;
  • (ii)Kusimamia mahitaji ya mafunzo katika masuala ya sheria kwa vitendo pamoja na usimamizi wa taarifaili kuhakikisha ufanisi katika uendeshaji kesi;
  • (iii)Kusimamia utendaji kazi wa kila mwendesha mashtaka, majukumu ya Jukwaa la Taifa la Haki Jinai, Kamati za kusimamia kesi na kuandaa ripoti na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka;
  • (iv)Kutekeleza mpango wa ulinzi kwa mashahidi;
  • (v)Kusimamia maandalizi ya miongozo inayohusiana na uendeshaji wa kesi za jinai na utekelezaji wa maelekezo ya jumla ya upelelezi;
  • (vi)Kusimamia utekelezaji wa maagizo yanayotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka kuhusiana na upelelezi wa kesi za jinai ili kuleta ufanisi;
  • (vii)Kusimamia uratibu wa upelelezi ili kuhakikisha ufanisi katika upelelezi unaoratibiwa namwendesha mashtaka;.
  • (viii)Kusimamia na kufanya kaguzi katika maeneo ambayo mahabusu wanahifadhiwa na kuchukua hatua stahiki;
  • (ix)Kufanya kazi na wadau wengine wa Haki Jinai ili kuwezesha uratibu wa kesi na ubadilishanaji wa taarifa; na
  • (x)Kuanzisha na kutunza mahusiano kati ya Ofisi, vyombo chunguzi na ushirikiano wa kitaifa na kimataifa.

Divisheni hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na Sehemu mbili (2) zifuatazo:

  • (i)Sehemu ya usimamizi wa kesi; na
  • (ii)Sehemu ya uratibu wa upelelezi.

Sehemu ya Usimamizi wa Kesi

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

  • (i)Kukagua na kufuatilia ubora juu ya huduma za uendeshaji kesi;
  • (ii)Kutathmini uhitaji wa mafunzo ya uendeshaji wa masuala ya sheria kwa vitendo na kuhakikisha ufanisi katika uendeshaji wa kesi;
  • (iii)Kuanzisha na kutunza orodha itakayosaidia kumbukumbu na ugatuzi wa kazi;
  • (iv)Kutathmini taarifa za kesi kulingana na miongozo na viwango vya taasisi;
  • (v)Kubaini masuala muhimu yanayojitokeza kwenye kesi zinazoamuliwa na kufanya uratibu na wadau wengine na kutoa mapendekezo;
  • (vi)Kutathmini utendaji kazi wa kila mwendesha mashtaka na kutoa mapendekezo;
  • (vii)Kuwezesha majukumu ya jukwaa la haki jinai;
  • (viii)Kuwezesha kamati za kusimamia kesi kwenye ngazi za wilaya, mkoa na kitaifa pamoja na majukwaa mengine;
  • (ix)Kutunza kanzidata na mfumo wa taarifa;
  • (x)Kuanzisha na kutekeleza mpango wa ulinzi wa mashahidi;
  • (xi)Kusajili na kutunza rejesta ya kesi zinazosajiliwa na au dhidi ya jamhuri;
  • (xii)Kurekodi kesi zilizosajiliwa mahakamani;
  • (xiii)Kuwasilisha nyaraka zinazohusiana na kesi za jamhuri;
  • (xiv)Kutunza majalada ya kesi zinazoihusu jamhuri;
  • (xv)Kuandaa na kutunza rejesta ya mawasiliano toka kwa umma katika kesi za jamhuri na zile zilizofunguliwa dhidi ya jamhuri; na
  • (xvi)Kupeleka nyaraka na mawasiliano mengine yanayohusiana na kesi.

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

Sehemu ya uratibu wa upelelezi.

  • Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:
  • (i)Kuandaa miongozo inayohusiana upelelezi wa kesi za jinai;
  • (ii)Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa miongozo inayotolewa na mkurugenzi wa mashtaka kuhusiana na upelelezi wa kesi za jinai;
  • (iii)Kuratibu upelelezi ili kuhakikisha ufanisi katika upelelezi unaoratibiwa na mwendesha mashtaka;.
  • (iv)Kufanya ufuatiliaji juu ya utekelezaji wa maelekezo ya jumla ya upelelezi ili kuleta ufanisi;
  • (v)Kusimamia na kufanya kaguzi katika maeneo ambayo mahabusu wanahifadhiwa na kuchukua hatua stahiki;
  • (vi)Kufanya kazi na wadau wengine wa haki jinai ili kuwezesha uratibu wa kesi na ubadilishanaji wa taarifa;
  • (vii)Kuwezesha majukumu ya jukwaa la haki jinai;
  • (viii)Kuwasiliana na ofisi za taifa za mashtaka wilayani na mikoani kwa lengo la kuratibu upelelezi;
  • (ix)Kuandaa na kusambaza miongozo kuhusu upelelezi na kusimamia upelelezi wa kesi za jinai;
  • (x)Kukagua na kufatilia ubora wa huduma zinazotolewa na divisheni;
  • (xi)Kutoa mapendekezo kuhusu utendaji kazi wa kila mwendesha mashtaka;
  • (xii)Kuratibu uendelezaji wa ujuzi kuhusu masuala ya kisheria ili kuhakikisha ufanisi katika upelelezi unaoongozwa na mwendesha mashtaka; na
  • (xiii)Kuanzisha na kudumisha mahusiano kati ya ofisi ya taifa ya mashtaka ,vyombo chunguzi na mashirika mengine ya kitaifa na kimataifa.
  • Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.