Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
Lengo: kutoa utaalamu na huduma za ununuzi na ugavi.
Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:
(i) Kushauri juu ya ununuzi , usimamizi wa vifaa na usambazaji wake;
(ii) Kufuatilia na kuhakikisha michakato ya ununuzi na taratibu zake zinafuatwa kwa mujibu wa sheria ya ununuzi wa umma;
(iii) Kuandaa mpango wa ununuzi wa mwaka;
(iv) Kununua, kutunza na kusimamia ugavi kulingana mahitaji;
(v) Kutunza na kusimamia usambazaji wa vifaa vya ofisi;
(vi) Kutunza na kuhuisha kumbukumbu za ununuzi na ugavi;
(vii) Kutoa huduma za sekretarieti kwa bodi ya zabuni;
(viii) Kuweka vigezo / viwango na kufuatilia uhalisia wa thamani ya bidhaa na huduma zinazonunuliwa; na
(ix) Kuandaaa mpango kazi , taarifa ya utekelezaji na bajeti ya ununuzi ya kitengo
Kitengo kitaongozwa na Mkurugenzi.