Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

TAWA imekabidhi jengo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilayani Kahama
02 Sep, 2020
TAWA imekabidhi jengo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilayani Kahama

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) mnamo tarehe 01/09/2020 imeikabidhiOfisi ya Taifa ya Mashtaka chini ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Biswalo Mganga jengo lililokuwa likitumika na mamlaka hiyo Kanda ya Kigosi lililopo Wilayani Kahama baada ya mapori waliyokuwa wakiyasimamia kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi ya Taifa, ambapo jengo hilo litatumika kuendesha kesi za jinai kwa lengo la kupunguza msongamano wa maabusu na wafungwa katika gereza la Wilaya ya Kahama linalohudumia na Wilaya za Mikoa ya jirani.

Akizungumza baada ya makabidhiano ya jengo hilo Kaimu Kamishna wa Uhifadhi nchini Bw. MabulaNyanda alisema kuwa kutokana na uhusiano uliopokati ya ofisi yake na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wamekuwa wakishirikiana katika masuala ya uendeshaji wa kesi za makosa yanayohusika na rasilimali za wanyamapori ambapo wameamua kuwapatia jengo hilo kwa muda ili waweze kusaidia jamii katika kesi mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka nchini Bw. Biswalo Mganga alisema kutokana na idadi kubwa ya watu walikuwa wakisafiri kwenda kupata huduma mkoani Shinyanga hali ambayo ilikuwa inachangia kuchelewa kutolewa kwa maamuzi ya kesi zao hivyo kusogezwa kwa huduma hiyo Wilayani Kahama itasaidia kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju alisema kuwa nchi haiwezi kuwa na amani pasipo na uwepo wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka hivyo ni jukumu la wadau wotekuungana katika kuhakikisha amani inatamalakiikiwemo kutoa elimu kwa jamii.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Katibu tawala wa Wilaya hiyo Bw. Timothy Ndonya alisema kuwa kwa sasa eneo lao lina idadi ya wakazi takribani milioni moja hali inayochangia kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu na makosa ya jinai kuongezeka pia, hivyo kusogezwa kwa ofisi hiyo Wilayani hapo kutasaidia kupunguza kero. Huku Kaimu Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga Davis Msangi akabainisha kuwa itasaidia kupeleka mashauri haraka ili haki itendeke.