Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akiwa katika picha ya pamoja washiriki wa Hafla ya Ufunguzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga iliyofanyika tarehe 16 Machi, 2024 katika eneo la Uzunguni.
Ufunguzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 16 Machi, 2024 katika eneo la Uzunguni.
Wanawake kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakikabidhi vifaa mbalimbali kwa baadhi ya wagonjwa wenye uhitaji kutoka Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ikiwa ni ishara mojawapo ya kufanya matendo ya huruma.
Wanawake kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakikabidhi vifaa mbalimbali kwa Mganga Mkuu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Bw. Stanley Mahundo vitakavyowasaidia wagonjwa wenye uhitaji waliopo katika hospitali hiyo ikiwa ni ishara mojawapo ya kufanya matendo ya huruma.
Muuguzi Mfawidhi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Bw. Stanley Mahundo akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma ambao wameshiriki kufanya Matendo ya huruma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma tarehe 6 Machi, 2024.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Miongozo ya Ushughulikiaji wa Kesi za Wanyamapori na Misitu pamoja na Kesi za Uvuvi Haramu kwa Waendesha Mashtaka na Wapelelezi katika hafla ya Uzinduzi huo uliofanyika tarehe 19 Februari, 2024 Jijini Arusha
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Miongozo ya Ushughulikiaji wa Kesi za Wanyamapori na Misitu pamoja na Kesi za Uvuvi Haramu kwa Waendesha Mashtaka na Wapelelezi katika hafla ya Uzinduzi huo uliofanyika tarehe 19 Februari, 2024 Jijini Arusha
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu (Katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi wa Saccos ya Mashtaka, viongozi wa Tughe, akifanya uzinduzi wa Mikopo kutoka Mashtaka Saccos Ltd. leo Januari 25,2024 katika Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka uliofanyika katika hoteli ya Lenana Jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanasheria wasio na Mipaka (Lwayers without Border) na washiriki waliohudhuria hafla fupi ya kusaini Makubaliano juu ya utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na usafirishaji haramu wa Binadamu. Makuabaliano yamefanyika leo January 24,2024 Jijini Mwanza.